Wakufunzi zaidi ya 20 wameweza kutoa mafunzo kwa Maafisa TEHAMA na Maafisa Habari wa Mamlaka za Mikoa na Hamshauri za Tanzania Bara kwa lengo la kuimarisha utoaji wa Taarifa kupitia tovuti za serikali ambazo zitakuwa na muundo mmoja wa utenegenezaji (Government Website Framework).
Pamoja na mafunzo hayo, wataalamu hawa wataziwezesha Taasisi zao kupitia Idara za Elimu Msingi na Sekondari kuweza kuimarisha utoaji wa elimu ya matumizi ya wavuti za serikali kama motisha kwa wanafunzi kupenda masomo yanaondana na ukuaji wa sayansi na Teknolojia.

Mmoja wa Wakufunzi Mwalimu Stanley Isaac Manyonyi (Kushoto Pichani) alikaririwa akisema kuwa katika mradi huu wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma utamsaidia kupanua wigo wa kuwafikia vijana walioko shuleni ili waweze kujengewa uwezo wa kuunda program ndogo ndogo ambazo zitawasaidia kuwapa ujuzi wa kutatua changamoto zilizopo katika jamii watakayoishi.
Aliendelea kutoa mfano wa mfumo mmoja wa tovuti za serikali uliotengenezwa na vijana wa kitanzania walio katika Wakala wa Serikali Mtandao, kuwa ni motisha kwa kuanza kufundisha vijana wadogo ili waanze kuzoea kutengenenza mifumo inayoendana na tamaduni ya mtanzania, na sio kutegemea mifumo iliyotengenezwa na watu wengine ambayo inatulazimisha kufuata tamaduni zao